Wajue Wapinzani wa Simba, Horoya A. C

Wajue Wapinzani wa Simba, Horoya A. C

Sports / 12th December, 2022Horoya AC players promised US$5,000 each if they win the CAF Confederation  Cup - Ghana Latest Football News, Live Scores, Results - GHANAsoccernet


Na Francis Mwacha.

Jina kamili ni Horoya Athletic Club ama Horoya Conakry kutoka Mji Mkuu wa Guinea Conakry, jina Horoya likiwa na maana ya Uhuru.


Klabu hiyo ilianzishwa mwaka 1975, moja ya timu yenye mafanikio makubwa zaidi nchini Guinea na mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu ya Guinea maarufu League 1 Pro, wametwaa taji hilo mara 20.


Horoya wamechukua ligi ya Guinea mara nane mfululizo, huku msimu huu wakiongoza ligi. Kweye michuano ya Afrika wameshiriki mara 18 Ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho huku wakishirki kombe la washindi mara Saba.


Hatua kubwa kuwahi kufika ni robo fainali ya ligi ya mabingwa mara mbili (2017,2018-19) na nusu fainali ya kombe la shirikisho mara moja ( 2019-2020) huku msimu uliopita waliishia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa.


Horoya A.C pia wamewahi kutwaa ubingwa wa kombe la washindi mwaka 1978 na kufika nusu fainali mara mbili ya michuano hiyo ambayo ilishaondolewa. Kwa Sasa wapo chini ya kocha Msenegal Lamine N'Diaye, wachezaji tegemeo Douda Camara, Mory Kante, Sekou Keita na wengine. 


Kwenye kikosi chao kuna wachezaji 12 wa kigeni, huku wachezaji Saba wakikipaga timu ya Taifa ya Guinea wakiwa na thamani ya Dola M1.23 (sawa na zaidi ya Tsh 2.8B) kwa mujibu wa mtandao wa Transfer market (Simba wana thamani ya Dola M1.68 sawa na zaidi ya Tsh 3.8B)


Hawa nao ni wekundu na weupe kama Simba SC, ingawa wanatumia na jezi za buluu pia.