Shomari Kapombe Kuikosa De Agosto.

Shomari Kapombe Kuikosa De Agosto.

Sports / 4th October, 2022

Kikosi  Cha Klabu ya Simba Sc Kinatarajiwa Kuripoti Kambini Leo Baada Ya Wachezaji Kupewa Mapumziko Ya Siku 1 Mara Tu Baada Ya Mchezo Wa Ligi Kuu Ya NBC PremierLeague Dhidi Ya Dodoma Jiji Fc Uliomalizika Kwa Simba Sc Kupata Ushindi Wa Goli 3-0.


Wachezaji Wote Wa Simba Sc Wanatarajiwa Kuripoti Kambini Kwa Ajili Ya Kuanza Maandalizi Ya Mchezo Wetu Wa Club Bingwa Barani Africa Dhidi Ya Clube Premeiro De Agosto Utakaopigwa Jumapili Ya Tarehe 9 October


MAJERUHI

Shomary Kapombe - Ameumia Nyama Za Paja Na Kwa Sasa Yupo Chini Ya Uangalizi Wa Daktari Wa Misuli Fareed Kassim.


Peter Banda - Ambae Alipata Majeraha Ya Bega Kwenye Mchezo Wa Dhidi Ya Malindi Fc Kisiwani Zanzibar Anaendelea Vizuri Na Atajumuika Na Wenzio Kuanza Rasmi Maandalizi Ya Mchezo Dhidi Ya Premeiro De Agosto.


Henock Inonga - Aliugua Ghafla Kabla Ya Mchezo Wetu Dhidi Ya Dodoma Jiji Lakini Hali Yake Imeimarika Kwa Sasa Na Atajiunga Na Wachezaji Wenzie Kwa Ajili Ya Kuanza Maandalizi Ya Mchezo Wetu Wakimataifa Jumapili.


Jimmyson Mwanuke - Alipata Majeraha Ya Goti Kwenye Mchezo Dhidi Ya Kipanga Na Yupo Chini Ya Uangalizi Wa Daktari Wa Misuli Fareed Kassim.


Pape Sakho - Alipatwa Na Msiba Wa Ndugu Yake Kwao Nchini Senegal Na Amerejea Nchini Salama Na Rasmi Atajiunga Na Wenzie Kambini Kwa Ajili Ya Kuanza Maandalizi Na Wachezaji Wenzie.


Wachezaji Wengine Woote Wapo Vizuri Na Rasmi Leo Kikosi Kitaanza Maandalizi Ya Mchezo Wetu Dhidi Ya Premeiro De Agosto.


Kikosi Cha Simba Sc Kinatarajiwa Kusafiri Kuelekea Nchini Angola Siku Ya Jumamosi Na Kitarejea Nchini Siku Ya Jumapili Mara Tu Baada Kumalizika Mchezo Dhidi Ya De Agosto.