Twaha Kiduku aendeleza ubabe amchapa Alex Kabangu

Twaha Kiduku aendeleza ubabe amchapa Alex Kabangu

Sports / 28th March, 2022

Bondia TWAHA KIDUKU amefanikiwa kubeba ubingwa wa UBO All-Africa Super Middleweight, baada ya kumchapa bondia mkongoman ALEX KABANGU.

 

KIDUKU, ameshinda kwa pointi za majaji wote watatu (Unanimous Decision) ambapo 'Score Cards' za majaji zilikuwa (80-72), (79-73) na (80-72)

 

KIDUKU, ameendeleza rekodi ya kutopoteza dhidi ya mabondia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, baada ya kuwachapa Mbiya Kanku, Sherif Kasongo, Tshibangu Kayembe na leo Alex Kabangu.