Kocha wa Simba SC Oliveira aelekea nchini kwao Brazil

Kocha wa Simba SC Oliveira aelekea nchini kwao Brazil

Sports / 24th January, 2023

Kocha Mkuu wa Simba Roberto Oliveira Arejea Kwao Brazil

Klabu ya Simba SC imesema Kocha Mkuu wa Klabu hiyo Roberto Oliveira ameondoka nchini kuelekea Brazil nchini kwao kwa shughuli binafsi za kifamilia na anatarajiwa kurejea mwishoni mwa mwezi huu.

Kocha Roberto anaondoka nchini ikiwa ni takribani siku 21 tangu aanze kazi kama Kocha Mkuu wa klabu hiyo baada ya kutambulishwa rasmi tarehe 23 januari,  2023.

Hatua hiyo inaifanya klabu ya Simba kurejea tena mikononi mwa Kocha Msaidizi  ambaye hivi karibuni alikuwa ndiye kocha Mkuu wa muda Juma Mgunda mpaka pale Kocha huyo Mbrazil atakaporejea tena.