Baleke awakosha Wanasimba
Mbio za ubingwa Ligi Kuu Ya NBC bado zinazidi kupamba
moto, ikiwa ni mzunguko wa 21, ambapo hapo jana timu mbili zilishuka dimbani.
Mnyama Simba alikuwa ugenini Katika Dimba la CCM
Jamhuri Jijini Dodoma dhidi ya Dodoma Jiji Fc.
Katika mtanange huo klabu ya Simba iliibuka na Ushindi
wa bao 1-0, bao lililowekwa na Mshambuliaji raia wa Congo Jean Baleke
aliyesajiliwa katika dirisha Dogo lililofungwa January 19 mwaka huu.
Licha ya Klabu ya Simba kuwakosa nyota wake muhimu
Cloatus Chama, Henock Inonga, Sadio Kanuote, Mzamiru Yasin, Peter Banda n.k
lakn haikumfanya ashindwe kuunguruma Dodoma mbele ya walima zabibu.
Kwa matokeo hayo Simba anaendelea kusalia katika
nafasi ya pili, akiwa amecheza mechi 21, alama 50 mkononi, wakipishana na Yanga
wenye alama 53 akiwa na mechi moja mkononi.
Siku ya Jana pia kulikuwa na Mechi kati ya Mbeya City
na Mtibwa Sugar katika dimba la Sokoine Jijini Mbeya. Mtanange ulimalizika kwa
bao 1-0, Mbeya City wakiondoka na alama 3, bao lililowekwa wavuni na kinara wa Magoli kwa timu ya Mbeya city
Sixtus Sabilo.
Leo January 23, 2022 Mbungi la NBC Premier League
linaendelea kama kawaida ambapo timu nne zitashuka dimbani kuwania alama 3.
Matajiri wa Chamazi, Azam FC watakuwa na kibarua
kizito mbele ya Singida Big Stars moja kati ya mechi bora sana kuitazama. Mara
ya mwisho timu hizi kukutana ni kwenye nusu fainali michuano ya mapinduzi Cup,
ambazo singida aliibuka na ushindi wa bao 4. Je, leo Azam atachomoa mbele ya
wabrazil pale Liti Singida?
Mchezo mwingine ni kati ya Mabingwa wa Tetezi Dar es
salaam Young Africans (Yanga), watakuwa dimba la Benjamin Mkapa Lupaso,
wakiwaalika Barcelona wa Bongo klabu ya Ruvu Shooting kutokea mkaoni Pwani
majira ya saa 1:00 Jioni.
Je, Yanga ataendeleza ubabe wake na kuchukua alama 3?