Fountain Gate Princess na Mbio za Ubingwa, Kushusha Vyuma 28

Fountain Gate Princess na Mbio za Ubingwa, Kushusha Vyuma 28

Sports / 23rd November, 2022


Mtendaji Mkuu wa Fountain Gate Sports Academy, Thabit Kandoro, amesema kuwa Fountain Gate imejipanga kutambulisha wachezaji, benchi la ufundi na viongozi watakaosaidia timu kutwaa ubingwa wa Ligi kuu ya Wanawake mismu wa 2022/2023.


“Hatushindwi Kusajili Mchezaji yeyote ndani ya Afrika ila kwasasa tumeamua kuwapa nafasi kubwa watoto wa kitanzania, ili waweze kuonekana kimataifa” amesema Thabit Kandoro.


Kandoro amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma, akielezea juu ya maandalizi kuelekea Fountain Gate Princess Day, inayotarajiwa Kufanyika Jumapili Nov 27, 2022 katika viwanja vya Fountain Gate Arena, Mlimwa C, Dodoma.


Miongoni mwa mambo makubwa yatakayofanyika siku hiyo ni utambulisho wa wachezaji wapya 28, watakaoenda kuongeza nguvu katika kikosi kilichopo, lakini pia kutakuwa na mechi ya kirafiki kati ya Fountain Gate Princess na mabingwa wa zamani wa Uganda, Lady Doves.


Hata hivyo siku hiyo itaambatanaa na mambo mengi ya kijamii kama vile kutembelea makundi yenye mahitaji Maalum.


Itakumbukwa kwamba Timu ya Wanawake Fountain Gate Princess msimu uliomalizika wa 2021/2022, wamefanikiwa kushika nafasi ya pili katika ligi ya wanawake nchini, ikitanguliwa na Simba Queens  huku Yanga Princess ikishika nafasi ya Tatu