Waziri Ummy awataka NIMR kuotesha Miti Dawa kila Halmashauri.
Waziri Wa Afya Ummy Mwalimu Jana 17 Mei, 2022. Katika Ufunguzi wa Kongamano la Utafiti
wa kisayansi ulio fanyika Jijini Dar es salaam. Waziri Ummy amewataka NIMR Kuwa na Mashamba
kiła Halmashauri watakayotumia kuotesha Miti Dawa.
"Nimewapa maelekezo NIMR, Nataka kuona Mashamba ya miti Dawa nchi nzima, kwa kuangalia
upatikanaji wa hizo dawa. Kwasababu hizi dawa zimetusaidia na zimetutibu" Alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amewataka NIMR kufanya utafiti kama Stafeli ni tiba ya Saratani. "Tunasikia Habari
mtaani kwamba Stafeli linatibu Saratani, Kwahiyo sasa ni NIMR Waingie kazini watupe utafiti Je
kweli Stafeli linatibu Saratani au halitibu Saratani"
Kwa upande wake Mkurugenzi wa NIMR Prof. Yunus Mgaya Amesema Kituo cha utafiti wa tiba asili
cha Mabibo kimeanza kazi. Prof Yunus, Ameahidi kutekeleza maagizo ya Waziri. “Tupo kwenye
mchakato wa kutafuta Ardhi kwa kushirikiana na Wizara Kwenye Mikoa kadhaa kulingana na hali
ya ikolojia ya Tanzania Ili kwenye yale Mashamba tulime miti ambayo tutakuwa tumeitambua
kupitia Elimu na maarifa waliyonayo Matabibu wetu wa kienyeji”. Alisema Prof Yunus