NIMR Yaagizwa Kufanya Tafiti Za Kusaidia Serikali Kufanya Maamuzi-Waziri Ummy

NIMR Yaagizwa Kufanya Tafiti Za Kusaidia Serikali Kufanya Maamuzi-Waziri Ummy

Health and Relationships / 6th June, 2022

Serikali  imeiagiza Taasisi ya Taifa ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kufanya tafiti zenye tija katika kusaidia kufanya Serikali kufanya maamzi.

Hayo ameyasema Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati akizindua Bodi ya Baraza la Ushauri ya Taasisi ya Taifa ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) jijini Dar es Salaam.

Ummy amesema katika utafiti huo ni pamoja na kufanya utafiti wa dawa za asili kutokana na kuwepo kwa maneno mengi kuwa zinatatibu ambapo NIMR inatakiwa kuja na ushahidi watafiti mitishamba hiyo.

Amesema kuwa kumekuwa na maneno tunda Sitafeli linatibu saratani ambapo NIMR kazi yake ni kuleta ushahidi wa kisanyansi.

Aidha amesema kuwa kuna dawa ya asili kapewa na kuamabiwa inatibu Ukimwi ndani ya siku saba ambapo kazi yake ni kupeleka NIMR au kwa Mkemia kwa ajili ya kuangalia sumu.

Amesema Baraza hilo liweze kushauri NIMR katika kufanya utafiti wenye tija katika kusaidia jamii kwa kutumia fedha nyingi kwa ajili ya matibabu.

Waziri Ummy amesema kutokana na tafiti ugonjwa wa malaria kuanza kutolewa chanjo ambapo ni matokeo ya utafiti yenye tija na kwenda mbali kwenye utafiti wa kudhibiti mazalia ya Mbu.

Hata hivyo sasa lazima kufanyike utafiti wa ugonjwa wa UTI kwani unachukua fedha nyingi za wananchi kwani kila wakipima wanaambiwa na UTI

Mkurugenzi Mkuu wa NIMR Profesa Yunus Mgaya amesema kuwa kumekuwa na ushirikiano na wizara ya afya katika kuendelea kufanya tafiti kwa ajili ya kukabiliana na magonjwa mbalimbali.

Profesa Mgaya amesema NIMR imekuwa ikifanya vizuri katika kufanya utafiti na kutambulika kimataifa hiyo ni kuonyesha kazi inafanyika na inaendelea kufanyika.


Mwenyekiti wa Baraza la NIMR Dk.Andrew Kitua amesema kuwa Bodi itaendelea kushauri NIMR ili kuhakikisha maagizo ya waziri yanafanyiwa kazi kwa kuleta tafiti zenye tija kusaidia serikali kufanya maamzi.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Ushauri la Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu waTaasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Profesa Yunus Mgaya akitoa maelezo kuhusiana na kazi za Taasisi hiyo wakati wa uzinduzi wa Baraza Ushauri la NIMR , Jijini Dar es Salaam.

Mganga Mkuu wa Serikali Dk.Aifelo Sichalwe akizungumza kuhusiana majukumu ya Taasis ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa Binadamu (NIMR) wakati wa Uzinduzi wa Baraza la Ushauri la NIMR jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)mara baada ya kuzinduliwa kwa Baraza la Ushauri la NIMR, Jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya mara baada ya kuzindua Baraza la Ushauri la NIMR, Jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Ushauri la NIMR mara baada ya kulizindua Jijini Dar es Salaam.