Tahadhari ya ugonjwa wa Homa ya manjano

Health and Relationships / 9th March, 2022

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametoa tahadhari ya kuzuka kwa ugonjwa wa Homa ya Manjano (Yellow Fever) ambapo amesema trh 03 Machi 2022 Wizara ya Afya ilipokea taarifa kutoka WHO hapa nchini ikielezea kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa homa ya manjano nchini Kenya.

 

Waziri Ummy ametoa wito kwa wananchi endapo wataona dalili zifuatazo kuwahi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya. Dalili za ugonjwa wa homa ya manjano ni pamoja homa, kuumwa kichwa, maumivu ya misuli na mgongo, mwili kutetemeka, kupoteza hamu ya kula, kusikia kichefuchefu na kutapika, mwili kuwa na manjano, kutokwa na damu sehemu za wazi kama mdomoni, puani, machoni na tumboni wakati mwingine damu huonekana kwenye matapishi na ugonjwa ukiwa mkali husababisha figo kufeli.