Serikali kuzindua kampeni ya Chanjo nchini
Wizara ya Afya imeweka mikakati ya kuongeza kiwango Cha uchanjaji wa chanjo ya polio ikiwemo mwongozo wa utoaji wa huduma za chanjo za kawaida katika kipindi Cha Uviko-19, utekelezaji wa mikakati ya kuinua huduma za chanjo ikiwemo mkakati wa kumfikia Kila mtoto yaani REC pamoja na kufikia watu wasiopata chanjo yaani PIRI katika Halmashauri 15
Aidha wizara inandaa matangazo ya rununga na redio yanayohamasisha wananchi kupelekea watoto kupata huduma za chanjo lakini pia wanahabari kusaidia katika uhamasishaji wa huduma za chanjo katika maeneo mbalimbali
Hayo ameyasema Afisa programu mpango wa Taifa wa chanjo kutoka wizara ya afya, Lotalis Gadau wakati akitoa mafunzo kwa wanahabari jijini Dar es salaam kuhusu mpango wa Taifa wa chanjo ya polio ambao unatarajiwa kuanza tarehe 18-21 mwezi huu.
Amesema wizara ina malengo na mipango mbalimbali ya kuhakikisha chanjo inamfikia Kila mtoto nchini;
"Tunampango wa kumfikia Kila mtoto kwa chanjo kwa usawa, kuongeza wigo wa utoaji huduma za chanjo kwa watu wote, kupunguza magonjwa yanayozuilika kwa chanjo kwa uanzishaji chanjo mpya ambazo hazitolewi kwa sasa na kutumia Teknolojia mpya katika kuboresha huduma za chanjo hasa maeneo ya mnyororo baridi, ukusanyaji takwimu na mawasiliano"
Kwa upande wake Mratibu wa Chanjo mkoa wa Dar es salaam, Juma Haule amesema Awamu ya kwanza walianza Kampeni ya chanjo ya polio katika mikoa inayopakana na chi jirani ambayo mlipuko huu ulitokea, ambayo ni songwe, njombe, Ruvuma na Kampeni hii awamu ya pili itaenda mikoa yote Tanzania bara pamoja na visiwani na dar es salaam ni Moja ya mkoa unaekwenda kufanya Kampeni ya chanjo ya polio
Kwa Upande wake
Kaimu Mkuu kitengo Cha Mawasiliano serikalini - Wizara ya Afya, Catherine Sungura amesema chanjo hiyo ni salama, Haina madhara yoyote na imethibitishwa na Shirika na Afya Duniani (WHO) hivyo watu watoe ushirikiano kupata chanjo hiyo.