MOI kwa kushirikiana na MUHAS yazindua Maabara ya mafunzo kwa watoa Dawa za usingizi na ganzi.
TAASISI ya Tiba ya Mifupa (MOI) kwa kushirikiana na Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), wamezindua maabara ya mafunzo ya dawa za usingizi pamoja na matibabu kwa wagojwa mahututi lengo likiwa ni kuongeza ufanisi kwa walimu na wanafunzi wa tiba hizo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Pascal Lugajo Kaimu Mshauri wa wanafunzi wa chuo MUHAS akimuwakilisha Makamu Mkuu wa Chuo alisema, chuo chetu kimejikita katika kutengeneza mitaala kwa ajili ya kusababisha sehemu za nyanja ya matibabu yenye mapungufu ya rasilimali watu katika tiba za usingizi na matibabu ya wagojwa mahututi.
Alisema, kama tulivyosikia rasilimali watu katika tiba za usingizi na matibabu ya wagojwa mahututi bado ipo chini sana kwahiyo kwa kuliona hilo tulianzisha mitaala kwa ajili ya madaktari wauguzi na kwa ajili ya mafunzo mbalimbali.
"Leo ni namna tofauti kwa sababu tunaona teknolojia jinsi ambavyo inaweza kusababisha mafunzo ya uhakika na kuongeza nafasi ya kutoa tiba nzuri kwa wagonjwa kwahiyo tunaishukuru MOI na MUHAS na wafadhili wetu tunatarajia kutokana na hii tutapunguza gepu la wataalamu wa usingizi na pia tutaimarisha mafunzo kwa wote waliopo ndani ya mafunzo na nje ya mafunzo.
"Takwimu zinaonyesha wanafunzi wanaohitimu MUHAS ni kunzia 15 mpaka 30 pia tumeendelea mbele na tumeanzisha mitaala kwa ajili ya wahitimu ambao wamekuwa wauguzi, kwa pamoja tumepiga hatua kubwa sana katika hili kwa kuweza kusaidiana na Wizara ya Afya katika kupunguza nakisi iliyopo katika wataalamu na tiba ya wagojwa mahututi", alisema Dkt Lugajo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini MOI Prf. Charles Mkonyi alisema maabara hizi zinatoa fursa ya kufundisha kwa wanafunzi ili waweze kujifunza katika mainzingira rafiki ili waweze kujifunza.
Alisema, kama wangekuwa wanaanza na mgojwa moja kwa moja basi likitokea kosa ina maana mgojwa amezulika kwahiyo hii ni nafasi ya kipekee sana ambayo imepatikana kutokana na maendeleo ya teknolijia ili kuweza kujifumza bila kutumia buguza, wala kumuweka mgojwa katika hatari ya kuweza kuathirika.
"Lakini pia maabara inaweza kutumika kwa watu ambao tayari ni wataalamu kwa ajili ya kuendeleza ujuzi wao siyo tuu kwa wanafunzi lakini pia kwa wataalamu kwa ajili ya kutumia vifaa hivi kwa kungoza na kukumbusha kuendeleza uwezo wao kwa kutoa huduma.
Naye Mkuu wa Idara ya Usingizi na Ganzi Edwin Ganzia alisema, malengo ya kuanzishwa kwa projeti hii ni kuongeza ufanisi wa walimu wa dawa za usingizi na ganzi pamoja na kujenga maabara zenye vifaa kwa ajili ya kufundishia wanafunzi kwa vitendo namna ya kufanya kazi kwa vitendo.
Alisema, zamani tulikuwa tunajifunza bila vitendea kazi tunaenda moja kwa moja kwa mgojwa kwa ajili ya mgojwa kumfanyia majalibio mgojwa na ina uwezekano mgojwa akapata madhara ili kuondokana na hilo kwa sasa tutajifunzia katika maabara zetu ili kuweza kusaidiana sisi kwa sisi.
"Ili kuondokana na mafunzo tuliyokuwa tunajifunza zamani tutajifunzia katika maabara zetu hizi ili kuweza kusaidiana kama uwezo wangu unaishia wapi na nani nimuite na nani anisaidie", alisema na kuongeza.
Alisema, wataalamu wa dawa za usingizi na ganzi wapo 75 nchi nzima, na tulisema wataalamu wanatakiwa 25 lakini hapa wapo wengi lakini wamegawanyika katika vipengele mbalimbali.