Rais Samia afanya uteuzi

Rais Samia afanya uteuzi

Politics / 6th June, 2022

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi watatu.

Taarifa ya uteuzi wa viongozi hao imetolewa siku ya jana Jumapili Juni 5, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imesema Rais Samia amemteua Dk Leonada Raphael Mwagike kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA).

Dk Mwagike ni Mtaalamu wa Ununuzi na Ugavi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Morogoro na uteuzi wake utaanza Julai, 21, 2022 baada ya Mwenyekiti aliyepo Balozi Dk Martern Lumbanga kumaliza kipindi chake cha pili Julai 20, 2022.

Pia amemteua Lutent Jenerali (Mstaafu) Samwel Albert Ndomba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Mzinga, Luteni Ndomba ameteuliwa kwa kipindi cha pili cha miaka mitatu kuanzia Juni, 2, 2022.

Vilevile amemteua Jaji Mustafa Kambona Ismail kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Masoko ya Mitaji na Dhamana Tanzania, Jaji Ismail anachukua nafasi ya Jaji Fredinand Wambali aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Rufani.

Uteuzi huu umeanza Juni, 2, 2022.