Halima Mdee: Kilichotokea ni uhuni

Halima Mdee: Kilichotokea ni uhuni

Politics / 12th May, 2022

Aliyekuwa mwanachama wa Chadema, Halima Mdee amesema hakukuwa na uhuru kwa wajumbe wa Baraza Kuu la chama hicho katika upigaji wa kura na kwamba, kilichofanyika ni uhuni.

 

Mdee ambaye amepata kuwa mbunge wa Jimbo la Kawe na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema, Bawacha, ni miongoni mwa makada walifukuzwa baada ya Bazara Kuu kubariki uamuzi wa Kamati Kuu ya Chadema kuwafukuza ndani ya chama kwa kukubali kwenda kuapishwa na kuwa wabunge kinyume cha matakwa ya chama hicho.

 

Matokeo ya jumla

 

Idadi ya wajumbe 423

 

Waliokubalina na maamuzi ya Kamati ya kuwafukuza Uanachama ni 413 sawa 97.6%

 

Wasiokubaliana na uamuzi wa Kamati kuu ni 5 sawa na 1.2%

 

Wasiofungamana na upande wowote ni 5 sawa na 1.2%