NCCR- Mageuzi limemsimamisha mwenyekiti wa chama chake James Mbatia

NCCR- Mageuzi limemsimamisha mwenyekiti wa chama chake James Mbatia

Politics / 21st May, 2022

Baraza Kuu la NCCR- Mageuzi limemsimamisha mwenyekiti wa chama chake James Mbatia na Makamu Mwenyekiti Bara Angelina Mtahiwa kushiriki katika shughuli zozote za chama hadi mkutano mkuu utakapoitishwa.

Uamuzi huo umefikiwa leo Jumamosi Mei 21,2022 kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo mgogoro kati ya viongozi na kujiuzulu kwa lazima.

Mjumbe wa Baraza Kuu na Mwenyekiti wa azimio hilo Joseph Selasini alisema pamoja na kusimamishwa kwa viongozi hao pia wamevunja Bodi ya Wadhamini ya NCCR na kuteua wajumbe wapya ambao watasajiliwa kwa mujibu wa taratibu.