Kinana ashiriki uchaguzi na kupiga kura kuchagua viongozi wa shina no 9, tawi la Masaki, kata ya Msasani Mkoani Dar es salaam.

Kinana ashiriki uchaguzi na kupiga kura kuchagua viongozi wa shina no 9, tawi la Masaki, kata ya Msasani Mkoani Dar es salaam.

Politics / 20th April, 2022

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana leo Aprili 19 , 2022 ameungana na Wanachama wenzake wa Shina Namba 9, Tawi la Masaki, Kata ya Msasani wilaya ya Kinondoni, Mkoani Dar es Salaam kufanya uchaguzi wa Viongozi katika Shina lao. Nafasi zilizopigiwa Kura ni Mwenyekiti wa Shina na wajumbe wanne wa Kamati ya Shina.


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana leo Aprili 19 , 2022 akiweka Karatasi ya kura katika boksi maalum la kupigia kura ya kumchagua Mwenyekiti wa Shina Namba 9 Tawi la Masaki, Kata ya Msasani wilaya ya Kinondoni, Mkoani Dar es Salaam.Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana wakifurahia Matokeo ya Uchaguzi pamoja na Wanachama wenzake wa Shina Namba 9, Tawi la Masaki, Kata ya Msasani wilaya ya Kinondoni, Mkoani Dar es Salaam.

Mshindi wa Kiti Cha Uenyekiti wa Shina Hilo Ndugu. Kizito Mahamba alieibuka kidedea baada ya kupata kura 108 akizungumza na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Tawi hilo.
 


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana leo Aprili 19 , 2022 akisalimia Wanachama wenzake wa Shina Namba 9, Tawi la Masaki, Kata ya Msasani wilaya ya Kinondoni, Mkoani Dar es Salaam wakati akiwasili katika uchaguzi wa Viongozi Shina namba 9 katika nafasi ya Mwenyekiti wa Shina na wajumbe wanne wa Kamati ya Shina.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana leo Aprili 19 , 2022 akizungumza na kufurahi Pamoja na Mwanachama Mwenzake wa Shina Namba 9 Bibi Christina Kilindo katika uchaguzi wa Viongozi Shina hilo katika nafasi ya Mwenyekiti wa Shina na wajumbe wanne wa Kamati ya Shina.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akiwa Katika Mkutano Mkuu wa Shina Namba 9 leo Aprili 19 , 2022Mwanachama wa Shina Namba 9 akipiga kura ya Kuchagua Viongozi wa Shina hilo ,Nyuma pichani ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akiwa katika mstari wa kupigia kura leo Aprili 19 , 2022.