Kinana apita kwa asilimia 100 umakamu Mwenyekiti CCM

Kinana apita kwa asilimia 100 umakamu Mwenyekiti CCM

Politics / 1st April, 2022

Wajumbe wa mkutano mkuu maalumu wa CCM wamemchagua Abdulrahman Kinana kuwa makamu Mwenyekiti wa CCM Bara kwa kura za ndiyo 1875.

 

Wajumbe waliopiga kura 1875, jura halali 1875, hakuna za hapana wala zilizoharibila

 

Matokeo hayo yametangazwa leo Ijumaa Aprili 1, 2022 na Dk Tulia Akson ambaye alikuwa msimamizi mkuu wa uchaguzi huo.

 

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara), Abdulrahman Kinana amepanda kukaa meza kuu kwenye nafasi yake huku mtangulizi wake Philip Mangula akikiachia rasmi kiti hicho na kumpisha.