Dkt.Tulia achaguliwa kuwa spika azoa kura zote 376

Dkt.Tulia achaguliwa kuwa spika azoa kura zote 376

Politics / 1st February, 2022

Mbunge wa Mbeya mjini Dkt.Tulia Ackson kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amechaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku akiwabwaga wapinzani wake wanane waliowania nafasi hiyo kutoka vyama mbalimbali.

Akitangaza matokeo baada ya wagombea kujieleza na kura kupigwa,Mwenyekiti wa uchaguzi huo William Lukuvi amesema,Dkt.Tulia amepata kura 376 kati ya kura 376 zilizopigwa na wabunge hao ambapo wagombea wenzake wote wamepata kura 0 kila mmoja.

“Kwa mamlaka niliyopewa namtanga Dkt.Tulia Ackson kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”amesema Lukuvi

Aidha Katibu wa Bunge Nenelwa Mwihambi amesema uchaguzi huo umefanyika kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri nya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Ibara ya 84 huku akitaja wagombea wa nafasi hiyo.

Ni bunge la 12 mkutano wasita kikao cha kwanza ambacho kimeanza kwa kumchagua Spika wa Bunge baada ya aliyekuwa spika wa Bunge hilo Job Ndugai kujiuzulu mnamo Januari  6 ,2022 ambapo wabunge wamemchagua Dkt Tulia Askon kushika nafasi hiyo.