China yasaidia Wizara ya mambo ya Nje Milioni 714/-

China yasaidia Wizara ya mambo ya Nje Milioni 714/-

Politics / 13th December, 2021

Serikali ya Jamhuri ya watu wa China imetoa msaada wa shilingi milioni 714 / - kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambapo msaada huo utakaotumika kuijengea uwezo Wizara ya Mambo ya Nje. 


Msaada huo umekabidhiwa Wizarani na Balozi wa China nchini Mhe . Chen Mingjian na kupokelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam .