Bunge la Tanzania sasa live
Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi amesema baada ya maboresho ya Studio ya Bunge na Kamati ya Uongozi ya Bunge kuridhia vikao vya Bunge vitaanza kurushwa live kuanzia kesho Jumanne Aprili 5, 2022.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma leo Jumatatu Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi, amesema bunge live litaanza kesho katika mkutano wa saba wa bunge la bajeti.