TRA yaondoa riba vyombo vya moto visivyo na usajili

TRA yaondoa riba vyombo vya moto visivyo na usajili

Business / 25th April, 2022

Mamlaka ya Mapato (TRA) imefuta adhabu na riba kwa vyombo vyote vya moto vilivyoingizwa nchini bila kufuata taratibu za forodha, huku wamiliki wakitakiwa kusajili rasmi vyombo vyao hadi kufikia Juni 30, 2022.

 

TRA imesema lengo la hatua hiyo ni kujenga ushirikiano na uhusiano mwema kati yao na walipa kodi sanjari na kuwapa motisha ya kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati pamoja na kuweka kumbukumbu au taarifa sahihi za umiliki wa vyombo hivyo.

 

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Aprili 25 jijini hapa, Mkurugenzi wa Huduma na elimu kwa mlipa kodi wa TRA Richard Kayombo amesema msamaha huo umetolewa kwa mujibu wa sheria ya usimamizi wa kodi inayompa mamlaka Kamishina Mkuu kusamehe riba na adhabu.

 

"Vyombo vilivyosamehewa ni vile vilivyoingizwa kwa njia zisizo rasmi, vilivyokusudiwa kwenda nchi za nje na vikatumika hapa kinyume cha taratibu, vilivyozidisha muda wa kukaa nchini na vilivyotumia msamaha wa kodi kinyume cha Sheria au kubadilishwa umiliki bila kufuata taratibu," amesema Kayombo.