Ruby International Kinara wa ulipaji kodi katika sekta ya madini
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela amempongeza Mkurugenzi wa kampuni ya Ruby International Ltd na Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mhe. Salim Alaudin Hasham kwa kampuni yake kuwa kinara wa ulipaji kodi katika sekta ya madini.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Ruby International ltd na Mbunge wa Jimbo hilo la Ulanga amesema anajivunia kuwa ni sehemu ya kuzalisha ajira kwani kwasasa anawafanyakazi zaidi ya 300 na anatarajia kutanua mgodi huo ili aweze kufikia ajira 700 mpaka 1000.
Migodi ya Epanko inachimba madini ya Spinel ambayo yanatumika kutengenezea thamani mbalimbali.
Mkuu wa mkoa Martine Shigela yupo wilayani Ulanga kwa ziara ya siku mbili kujionea miradi mbalimbali ya maendeleo inavyokwenda na kuhakikisha fedha za serikali zinatumika ipasavyo.