FCC yaimarisha ushirikiano na ZFCC, zajipanga kudhibiti uingizaji na uzalishwaji wa bidhaa bandia.

Business / 25th May, 2022

Tume ya ushindani FCC kwa kushirikiana na Tume ya ushindani halali ya Zanzibar ZFCC zimejipanga kudhibiti uingizaji na uzalishwaji wa bidhaa bandia ili kuchochea uchumi utakaolinda soko la ndani na Kumlinda mlaji

 

Ameyasema hayo leo 25 Mei, 2022 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC) William Erio wakati wa kuhitimisha ziara ya kikazi ya siku tatu kwaajili ya kutembelea  Tume ya Ushindani Tanzania (FCC) ikiwa na lengo la kuimarisha mahusiano na kuangalia namna bora ya kutekeleza majukumu yao

 

"Suala la bishara  si suala la muungano, kwahiyo sisi FCC tunashughulika na masuala haya ya kibiashara kwa maana ya kushajihisha ushindani, kulinda washindani katika shughuli zao na kumlinda mlaji kwa Tanzania bara ambapo na wenzentu wanafanya hivyohivyo kwa upande wa Tanzania Zanzibar"

 

"Pamoja na kwamba suala la biashara si suala la muungano lakini muingiliano kibiashara kati ya pande hizi mbili za muungano ni mkubwa  kwanza kwa wafanyabiashara wenyewe lakini pia wawekezaji ambao wamewekeza katika pande zote mbili za muungano"

 

Aidha Mkurugenzi huyo alisema Serikali ya awamu ya sita imejikita katika kuimarisha uwekezaji Kama njia mojawapo Kuu ya kuleta mitaji na kukuza uchumi wa nchi yetu Kama vile inavyofanya serikali ya awamu ya nane kule Tanzania Zanzibar.

 

Pia Erio alisema wanajipanga zaidi katika kuhakikisha kwamba nchi yetu inanufaika na soko la Afrika Mashariki kwasababu sisi wote ni sehemu ya Afrika mashariki.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani halali ya biashara Mohammed Sijamini amesema  kuwa Zanzibar inaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na kufanya mapitio ya baadhi ya sheria ikiwemo sheria ya maendeleo ya viwanda ambayo itawezesha wananchi kunufaika  na bidhaa zinazozalishwa viwandani.

 

"Kwa upande wa Zanzibar kuna jitihada kubwa zinafanyika za makusudi kwake Mhe. Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi kwa kuweka mazingira bora ya biashara na kudhibiti ushindani"

 

Aidha Sijamini alisema

Kuna sheria nyingi wanazifanyia mapitio mfano sheria ya maendeleo ya viwanda ambapo wameamua kuwepo kwa sheria hiyo.

 

Miongoni mwa mambo ambayo ZFCC imejifunza kutoka Tume ya Ushindani Bara ni pamoja na masuala ya ukaguzi na udhibiti wa bidhaa bandia ,taratibu za kanuni na sheria ,na masuala ya muunganiko baina ya kampuni.