Equity Bank (t) imezindua rasmi tawi lake katika wilaya ya Kahama mkoa wa Shinyanga

Equity Bank (t) imezindua rasmi tawi lake katika wilaya ya Kahama mkoa wa Shinyanga

Business / 26th May, 2022

  

Benki ya Equity  (T) Jana Jumatano 25 Mei, 2022  imezindua rasmi tawi lake jipya wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga. Tawi hili lipo Kahama mjini jengo la MACHALI TOWER na huduma zote za kibenki zitakuwa zinapatikana kuanzia siku ya jumatatu mpaka jumamosi. Hatua hii ni moja ya muendelezo wa benki kuongeza wigo wake wa upatikanaji nchini ili kuweza kuwafikia wateja wote Tanzania na kuhakikisha kuwa tunatimiza dhamira yetu ya kubadilisha maisha ya kila Mtanzania. Uzinduzi huu umefanywa na mkuu wa wilaya ya Kahama ndugu Festo Kiswaga ukishuhudiwa na baadhi ya wageni waalikwa. 


Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tawi hilo, mkuu wa wilaya alisema,   “Hatua hii itatuongezea wigo wa mtandao wa utoaji huduma zetu ambazo ni nafuu zaidi nchini na hivyo kuendana na lengo letu la kukomboa Watanzania kiuchumi kwa kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anatumia mifumo rasmi ya kifedha (financial inclusion). Pia msemaji wa benki alisema “Akaunti zetu hazina makato ya mwezi na tuna viwango bora kabisa vya riba sokoni. Pia kupitia tawi hili huduma nyingi  zitatolewa ikiwemo kufungua akaunti na kupata mikopo mbalimbali” amesema Betty Kwoko. 



 


  


Kuhusu Benki ya Equity Equity Bank (T) ni Benki yenye matawi 15 nchini ikiwa na zaidi ya wafanyakazi 1200 ukiwa ni moja ya uwekezaji mkubwa zaidi ulioanzia nchini Kenya na baadaye kusambaa katika nchi nyingine za Afrika ikiwemo Tanzania, Uganda, Ethiopia, Congo-DRC, Rwanda na Sudan ya Kusini. Kwa maelezo zaidi: grace.majige@equitybank.co.tz, 0688988110.