Zaidi ya Mil. 150 zatolewa kwa washindi NMB MastaBata Kote Kote.

Zaidi ya Mil. 150 zatolewa kwa washindi NMB MastaBata Kote Kote.

General / 6th January, 2023



Meneja wa Benki ya NMB kanda ya Kaskazini Dismas Prosper (kushoto) akimkabidhi kadi ya pikipiki mshindi wa Pikipiki katika droo ya NMB Mastabata kote-kote, Ally Asbat (katikati) kutokea jijini Tanga. Kulia ni Meneja wa huduma kwa wateja wa Benki ya NMB tawi la Madaraka – Tanga, Getrude Mahendeka. Benki ya NMB imeshatoa Pikipiki kumi mpaka sasa zikiwa ni zawadi kwa wateja wa NMB wanaofanya malipo kupita NMB mastercard au Mastercard QR katika msimu huu wa Mastabata. (Na Mpiga Picha Wetu).


Benki ya NMB imeanza mwaka kwa kusambaza upendo kupitia kampeni ya #MastaBataKoteKote kwa kumzawadia mshindi wa pikipiki mpya aina ya boxer wa droo ya sita, Ally Asbat Abdallah kwenye droo ya pili ya mwezi iliyofanyika mkoani Tanga.

Mpaka sasa, kampeni hii imeshawazadia wateja wake jumla ya Sh. Mil 150,500,000 kwa washindi 623 na kabla ya jana, boda boda 9 ziliishanyakuliwa; 7 kwenye droo za wiki na 2 kwenye droo ya kwanza ya mwezi iliyofanyika Iringa. Zikijumulishwa na 2 za jana, jumla inakuwa pikipiki 11 zenye thamani ya zaidi ya 33m/- huku nyingine tatu zikiwa zimebakia kwa ajili ya droo za kila wiki zilizobaki.

Zimesalia siku 25 tu kuelekea grand finale ambapo tutashuhudia wateja 8 wakijishindia safari ya kwenda Dubai kwa siku 4 huku benki ya NMB ikiwalipia kila kitu.

Usiache kadi yako ya NMB mastercard nyumbani kufanya malipo ya matumizi yako au kwa kuscan QR kujiweka katika nafasi ya kuweza kuwa mmoja wa washindi wa #MastaBataKoteKote.