NMB ‘Masta Bata Kotekote’ msimu wa nne, Zaidi ya milioni 300 kutolewa
Na Taji Silasi
Benki ya NMB imezindua msimu wa nne wa Masta Bata kotekote
wenye lengo la kuwahamasisha wateja wake kutumia kadi kufanya malipo.
Hayo yamesemwa leo Nov 11, 2022 na Meneja wa NMB Kanda ya
Dar es Salaam Donatus Richard wakati akichezesha droo ya kwanza ya Masta Bata Kotekote
msimu wa nne ambapo mshindi wa mwanzo amepewa bodaboda huku washindi wengine 75
wakipewa fedha taslim shilingi 100,000.
Aidha Richard amesema droo hiyo itatolewa kila wiki ambapo
mshindi atapata fedha taslim na wengine kushinda bodaboda, huku akiongeza kuwa
droo hiyo kwa mwezi mshindi atapata bodaboda mbili na fedha taslimu kutolewa
kwa washindi wengine. Grand finale washidni saba watapata fursa ya kwenda Dubai
na Zanzibar ambapo kila mshindi ataweza kwenda na mwenzake au rafiki katika
safari biyo.
Amesema Benki ya NMB imekuwa ikiendelea kuwahamasisha
watanzania kupitia kampeni mbalimbali kutumia Zaidi kadi kufanya malipo badala
ya mutumia fedha taslim ambapo pia kadi hiyo hutumika kufanya malipo ndani na nje
ya nchi.
“Mnafahamu kwa muda mrefu tumekuwa na kampeni mbalimbali za
kuhakikisha watanzania wanatumia Zaidi kadi na tumekuwa tukishirikiana na
wenzetu wa Master card kuhakikisha tunaendeleza utamaduni huu wa kuitumia kadi badala ya pesa taslimu.”
“Ukiwa na kadi yako unaweza kuitumia popote ukwia ndani au
ukienda nje ya nchi.” Ameongeza Richard.
Katika hatua nyingine ametoa wito kwa watanzania kuendelea
kutumia master card kufanya malipo ili kujiweka katika nafasi ya kushinda zawdi
hizo za Masta bata kotekote
zilizoandaliwa msimu wa nne.
Naye Meneja Mwandamizi Idaraya Biashara za Kadi, Manfred
Kayala amesema droo hiyo itachezeshwa kwa Zaidi ya miezi mitatu na kuwasisitiza
wateja kuendelea kutumia zaidi kadi katika kufanya malipo.
“Wateja wetu mnashauriwa kutumia kadi badala ya kutumia pesa
taslimu, ambayo tunajua kwamba pesa taslimu kutembea nazo inakuwa ni
changamoto, zoezi hili tutakuwa tunalifanya kw takribani miezi Zaidi ya mitatu,
na washindi nmbalimbali watapatikana”.