HALOTEL TZ yampatia gari jipya mshindi wa promosheni ya 7BANG BANG
Mkurugenzi wa Biashara Bw: Abdallah Salum mshindi mkuu wa gari mpya aina ya IST Ms. Scolastica Sostenes Haule, pamoja na mme wake kutoka mkoa wa Songea kwa pamoja wakifungua gari mara baada tu ya hafla ya makabidhiano rasmi ya gari hilo yaliyofanyika katika jengo la Palm Village Mall iliyoko pembezoni mwa Mikocheni B Dar es Salaam.
Kampuni ya Mawasiliano nchini ya Halotel Tanzania PLC imekabidhi zawadi
kwa mshindi mkuu aliyejishindia gari aina ya IST Mpya wa draw kubwa ya mwisho
ya promosheni ya wateja iliyokuwa na jina la 7bang bang.
Akizungumza
leo Januari 5, 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla makabidhiano ya gari
jipya aina ya IST Mkurugenzi wa Biashara wa Halotel Bw; Abdallah Salum, amesema,
“Leo hii, tuna mshindi aliyebahatika kujishindia gari jipya kabisa kwa
kushiriki katika shindano letu la promosheni ya 7 bang bang. Tumeona itakuwa
vizuri ikiwa zawadi hii ya gari ikakabidhiwa wakati tukiwa tunamalizia msimu wa
sikukuu ukiwa sambamba na kuwashukuru wateja wetu wote kutumia huduma za
Mawasiliano kutoka Halotel sambamba na kuadhimisha miaka 7 kutoa huduma hapa
nchini”.
Katika
tukio hili la makabidhiano, zawadi kubwa kuliko zote ya gari jipya aina ya IST
ilikabidhiwa kwa mshindi.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi rasmi gari hilo, Mkurugenzi wa Biashara Halotel Bw.
Abdallah Salum amesema siku ya leo wanayo furaha sana kuweza kumkabidhi mteja
wao ambaye ni mshindi mkuu wa gari mpya aina ya IST katika droo kubwa ya mwisho
ya promosheni iliyokuwa na jina la 7 bang bang.
“Bi Sholastika Sostenes Haule. Napenda kukupa pongezi kubwa sana na
unavyochukua gari lako, ninakuasa kutumia zawadi hii ambayo ni fursa adimu,
katika kupiga hatua kimaisha na isiwe mwisho wa jitihada zako. Hii iwe hatua
kwako, kukufanya uendelee kuweka bidii ili uendelee kupanda zaidi kimaisha.”
Aidha
Bwana Abdallah Salum, ametumia fursa hiyo kuwahimiza wateja wao waendelee
kutumia mtandao wa Mawasiliano wa Halotel ambao unaendelea kuwa na ubinifu
kuhakikisha kila mteja anafurahia huduma za mawasiliano kwa ubora wa hali juu
kutoka Halotel.
Kwa
upande wake, Bi Sholastika Sostenes Haule aliishukuru kampuni ya Halotel, na
kuwasihi wateja kuendelea kutumia mtandao wa Halotel na kushiriki katika
promosheni zinazotolewa kampuni ya Halotel ili waweze kujishindia zawadi
mbalimbali zinazokuwa zinatolewa kupitia promosheni hizo.
Sambamba
na tukio hilo la kukabidhi zawadi ya gari kwa mshindi, Kampuni hiyo imetumia
fursa hiyo kufanya uzinduzi wa duka jipya na la kisasa linalopatikana Palm
Village Mall iliyopo kando ya barabara ya Mwai Kibaki Mikocheni, Dar es Salaam
ambapo wateja wa Halotel sasa watapata huduma zote za Halotel katika Duka hilo.
Duka
hilo lililoboreshwa kwa njia ya kidigitali litatoa huduma zote zitakazojumuisha
huduma ya kusajili laini mpya na kusalijili upya namba za simu kwa mfumo wa
alama za vidole, ubadilishaji wa laini kutoka 3G kwenda 4G, Huduma za vocha
(elektroniki na kukwangua) uthibitishaji wa namba za simu, huduma za HaloPesa,
bidhaa za Halotel kama router na huduma zote za ziada na za baada ya mauzo.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Biashara Bw Abdallah Salum amesema
“uzinduzi wa duka hilo jipya unaenda sambamba na mkakati wa Halotel wa
kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja na kutimiza ahadi yake ya kuwapatia
wateja fursa ya kupata bidhaa na huduma kwa ukaribu na urahisi zaidi”.
“Tunapenda
kuwakaribisha wateja na watanzania wote kwa ujumla katika duka letu la Halotel
hapa Palm Village Mall kuweza kupata na kufurahia huduma bora za Halotel katika
duka hili” aliongeza Bw. Abdallah.
Promosheni hiyo ya “7 bang bang” iliendeshwa kwa wiki 10 na kuwapa fursa wateja wote wa Halotel ambao wamekuwa wakiwaunga mkono kwa kutumia huduma zao kwa miaka saba (07) ya utoaji huduma bora za M.awasiliano hapa nchini. Tangu kuanza kwa promosheni hiyo ya bahati nasibu zaidi ya washindi 140 wameweza kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo Vocha yenye thamani mpaka laki moja, Simu janja aina ya Samsung Galaxy A53 na A73, Televisheni janja zenye inchi 50.
Mkurugenzi wa Biashara Bw: Abdallah Salum mshindi mkuu wa gari mpya aina ya IST Ms. Scolastica Sostenes Haule, pamoja na mme wake kutoka mkoa wa Songea kwa pamoja wakifungua gari mara baada tu ya hafla ya makabidhiano rasmi ya gari hilo yaliyofanyika katika jengo la Palm Village Mall iliyoko pembezoni mwa Mikocheni B Dar es Salaam.