Zaidi ya Miradi 1,000 ya Maji kujengwa

Zaidi ya Miradi 1,000 ya Maji kujengwa

General / 15th October, 2022

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga amesema Serikali inajenga zaidi ya miradi 1,000 katika maeneo mbalimbali kote nchini ili kuwasogezea huduma ya majisafi na salama wananchi wake.

Mhandisi Sanga amesema hayo wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji wa Mbalache-Lupombwe.

“Kila kona ya nchi hii kuna mradi unajengwa na niwahakikishie miradi mingi inayojengwa kipindi hiki ni miradi yenye ubora mzuri na hata kwenye Mbio za Mwenge mwaka huu miradi iliyokaguliwa ilipongezwa na viongozi wa mbio za mwenge,” amesema Mhandisi Sanga.

Mhandisi Sanga amewapongeza wataalam Wizara ya Maji kwa kuhakikisha ubora wa miradi lakini pia aliwapongeza Viongozi wa Serikali na Chama cha Mapinduzi Wilayani Makete kwa jitihada zao, ufuatiliaji na usimamizi wa ujenzi wa miradi ya maji wilayani humo.