Watanzania Mbioni Kupata Mkopo wa Simu Janja (Smartphone)

Watanzania Mbioni Kupata Mkopo wa Simu Janja (Smartphone)

General / 7th January, 2023

Nape Nnauye Waziri mpya wa Habari – Bongo5.com

Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema Serikali iko mbioni kutafuta namna ya kumuwezesha Mtanzania wa kawaida kumudu gharama za kununua simu janja (Smartphone) kwa kukopeshwa ili awe analipa kidogokidogo.


Amesema hayo wakati akizindua mnara wa mawasiliano ya simu katika kijiji cha Kinenulo Mkoani Njombe uliojengwa kupitia ruzuku inayotolewa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote ( UCSAF ) huku akibainisha kuwa malengo ya Serikali ni kuhakikisha kila Mtanzania kokote alipo anaunganishwa na huduma ya mawasiliano.

Nape amesema hivi sasa wanafanya mazungumzo na makampuni ya simu β€œNa Mimi kwa sababu naipenda kazi yangu nimeshaanza kuhangaika tumebanana na makampuni ya simu tunatafuta utaratibu ambao makampuni ya simu na watoa huduma wengine wataleta simu walau iwe ni kwa mkopo mtu alipe taratibu lakini aipate huduma aanze kutumia "

β€œ Mtu wa kawaida kuchukua laki tatu ukaenda kununua simu kidogo ngumu lakini tukimwambia weka Elfu 30 upewe simu ya laki tatu alafu utakua unakatwa kidogo kidogo hata kama ni kwa mwaka mzima , huduma unapata, umepata kwa bei ndogo na maisha yanaendelea na maagizo hayo ameyatoa Rais Samia "