Wanawake waaswa kumuiga kwa vitendo Rais Samia

Wanawake waaswa kumuiga kwa vitendo Rais Samia

General / 23rd September, 2023


Na Iddy Lugendo 


KUPAMBANA na kuonyesha wanawake wanaweza bila kumtegemea mwanaume, tufuate mfano mzuri wa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye anaonyesha kwa vitendo kwamba wanawake tunaweza ,na atakayebisha hilo huyo atakuwa ana chuki zake binafsi


Awali Katibu wa TAWOMA Salma Ernest ameelezea mafanikio ya chama hicho katia kipindi cha miaka miwili ya Rais Samia huku akisema,chama kimeweza kufanya programu mbalimbali za kujikwamua kiuchumi kupitia sekta ya Madini.


Amesema, chama hicho kina wanachama mikoa 21 ya Tanzania na wanatarajia kuongeza mikoa mingine lakini  pia wapo katika wilaya 41 na wana matawi au programu ya vijana ambao mpaka sasa wana vikundi 14 vya vijana ambao wamejiajiri kwa kutengeneza vitu mbalimbali kwa kutumia madini yenye ubora wa chini  ambayo hayana soko.


Aidha amesema chama hicho kinaendesha vikundi  34  vya kusaidia jamii  ambapo 17 vipo Tanga na 12 kutoka Morogoro vijijini ambavyo hukopeshana na hivyo kumudu kusaidia familia .


Katika hatua nyingine amesema chama hicho kinatimiza miaka 25 ya chama chao na wamekuja na programu iitwayo Malkia wa Madini ambapo wameandaa programu migodini pamoja na afya ya mama na mtotom,utunzaji umbuumbu ,eimu ya miopo,vifaa  na tenoojia ambapo pia wameungana na maundi maaum waemavu ambao wapo nao wenye programu hiyo.


Amesema,Sherehe hizo zitafanyika Septemba 29 mwaka  huu ambapo watakuwa na matembezi ya Hisani kutoka ukumbi wa Halmashauri mpaka kwenye viwanja vya maonesho huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Maendeeo ya Jamii,Jinsia na Maundi Maalum Dkt.Dorothy Gwajima huku uzinduzi wa proramu hiyo ukipangwa kutafanyia Otoba 30 .


Katika sherehe hizo mgeni rasmi atazindua  na kumvisha taji malkia wa Madini Tanzania 2023.