Walimu 1,362 Wafunguliwa Mashauri ya Utoro
Tume ya Utumishi wa Walimu kupitia kwa mtendaji wa
tume hiyo, Mwalimu Paulina Nkwama amesema kuwa suala la utoro kwa walimu bado
ni pasua kichwa, kutokana na uwepo wa makossa mengi ya utoro miongoni mwa
walimu.
Mwalimu Nkwama
ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 27,2022
Jijini Dodoma, juu ya mafanikio yaliyopatikana
katika tume hiyo toka Rais Samia Suluh Hassan aingie madarakani.
“Mashauri 1365 sawa na 69.8% yametokana na
utoro, walimu 919 sawa na 56%
wamefukuzwa kazi, mashauri 260 sawa na 13.3% yalihusu kughushi vyeti, 119 sawa na 6.1% yalihusu mahusiano ya kimapenzi baina ya walimu na wanafunzi, Mashauri 98 sawa na 5% yalihusu ukaidi, mashauri 66 sawa na 3.4% yalihusu ulevi” Amesema Mwalimu Nkwama
Mwalimu Nkwama, amesema
kuwa walimu 16,749, wwa shule za msingi 8,949 na 7,800 wa shule za sekondari waliajiriwa
, huku walimu 15,802 walisajiliwa 8,512 wa shule za msingi na 7,290 wa shule za
sekondari.
Katika hatua nyingine
Mwalimu Nkwama amezungumzia suala la maadili ya walimu wawapo kazini ambapo amesema
kuwa katika kipindi cha mwezi machi 2021 hadi DSeptemba 2022 jumla ya makosa ya
kinidhamu 1952 yamefikishwa kwenye mamlaka husika kwa mujibu wa kifungu cha 13,
kifungu kidogo cha pili kwaajili hya kuchukuliwa
hatua za kinidhamu.
“Kamati ya nidhamu inatekeleza majukumu yake kwa
haki na usawa bila kubagua kosa lolote atakalofanya mwalimu na likathibitika
kwasababu unaweza ukamzushia mtu kwamba mwalimu amefanya kosa kumbe nin sababu yupo makini kwenye kazi yake”
Tume ya Utumishi wa
Walimu, (Teaching Service Commision)TCS, imeanzishwa kwa mujibuwa sheria sura
namba 248, sheria namba 25 ya mwaka 2015, Tume hii ipo chini ya TAMISEMI, ambapo ilioanzishwa
ili kuongeza ufanisi katika kuwahudumia walimu katika masuala ya ajira,
kuwasajili, kuwathibitisha kazini, kushughulikia mafao yao pamoja na kusimamia
maadili na nidhamu kwa walimu na maendeleo yao wawapo shuleni.