Wafanyabiashara Wapatiwa Mafunzo Umuhimu Anwani za Makazi

General / 13th December, 2022

Wizara ya habari, mawasiliano na Teknolojia ya habari imeendesha mafunzo kwa wafanyabiashara kuhusu  umuhimu wa kutumia anwani za makazi kwenye biashara zao kwa kuwa zina manufaa ya kijamii na kiuchumi.


Hayo yamebainishwa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Aloyce Mogofi huku akisema kikao kazi hicho ni muhimu kwa kuwa kinalenga kujenga uelewa wa pamoja katika kuhamasisha matumizi ya anwani za makazi.


“Ukitumia anuani ya makazi ni rahisi kumuelekeza mtu akakupata kwa haraka kwasababu atajua mtaa wako lakini pia atajua namba ya nyumba unayokaa itakurahisishia wewe kama mfanyabiashara kufikiwa bila shida na wateja wako,”amesema Mogofi.


“Lazima tuelewe kuwa maendeleo ya biashara yanayegemea zaidi mfanyabiashara anayejitambua na kukubali kwenda na wakati,”ameongeza.

Awali, Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Clarence Ichwekeleza, amesema kuwa mfanyabiashara mwenye anwani kamili inarahisisha kufikiwa kwa haraka.


“Anwani kamili lazima iwe na jina la mtaa, jina la barabara, namba ya nyumba na kata namba zake zimewekwa ambazo ni postikodi, ni muhimukufikiwa kwa urahisi kupata huduma za kijamii na kiuchumi,”amesema


IMG-20221213-WA0124

Kwa upande wake Mtaalamu wa Tehama, Wizara ya ardhi,Nyumba na maendeleo ya makazi Anord Mkude,akitoa mafunzo kuhusu umuhimu wa utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi kwenye mafunzo hayo amesema umuhimu wa utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi nchini ni kuwezesha mipango na tafiti kufanyika kwa tija, kuongeza vyanzo vya fedha , kuimarisha usalama ,kuwezesha utoaji , upatikanaji na upelekaji wa huduma za bidhaa hadi mahali husika.

Mkude ametaja manufaa mengine kuwa ni kusaidia wawekezaji kufanya maamuzi kabla ya kuamua kufanya uwekezaji na kuwezesha biashara mtandao kufanikiwa hali itakayo inua fursa ya uchumi wa kidigitali.

“Jamii inapaswa kutambua kuwa postikodi ni utaratibu wa kitaalam unaotumika kutenga maeneo ya makazi wakati amwani za makazi ni miundombinu ambayo Kwa Pamoja inatambulisha mahali halisi mtu ama kitu kilipo,aina hii ya utambulisho inaundwa na vitu vikuu vitatu ambavyo ni namba ya anwani,jina la barabara na postikodi,”amefafanua
IMG-20221213-WA0123

IMG-20221213-WA0115