Ufafanuzi NECTA Kutotangaza Shule Bora
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa uamuzi wa kutotangaza shule na wanafunzi bora katika matokeo ya mwisho ya mitihani kwa darasa la Saba na kidato cha Nne, ni kutokana utata wa namna ya kuzitathmini shule na wanafunzi hao.
"Unakuta shule inawanafunzi 100 waliomaliza kidato cha nne, nyingine inawafunzi 20. Ile yenye wanafunzi 100 kwenye matokeo inapata A 70 na 30 waliosalia hawana A. Upande wa pili shule yenye wanafunzi 20 inapata A zote, ukiangalia kwa wastani inamaana shule yenye wanafunzi 20 itatangazwa kuwa shule Bora, hii haiko sawa" amesema Mkenda.
Mkenda amesema hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati akitolea ufafanuzi juu ya uamuzi huo uliofikiwa na baraza la mitihani kujiondoa katika jukumu hilo la kutotangaza shule na wanafunzi bora mwaka huu.
Amesema uamuzi huo ulifikiwa mwezi Novemba mwaka jana, wakati wa kikao cha Baraza la Mitihani la Taifa NECTA, ambapo baraza halikutngaza shule Bora katika matokeo ya darasa la Saba, yaliyotangazwa Disemba 1,2022 pamoja na matokeo ya kidato cha nne mwaka 2022.
Aidha, Mkenda amesema kuwa takwimu zote zinazoonesha shule iliyopata alafa za chini na alama za juu zipo hadharani hivyo mtu yeyote anaruhusiwa kupitia na akaona shule iliyofanya vizuri kuliko zote.
"Sio kama nchi nyingine ambazo zinaficha Takwimu, kwetu sisi takwimu hazijafichwa zote zipo handharani, kama mtu anataka kuona shule ipi bora na ili haijafanya vizuri basi anaweza kuangalia" amesema Mkenda