TMRC yaorodhesha Hati Fungani ( Bond ) sokoni awamu ya nne

TMRC yaorodhesha Hati Fungani ( Bond ) sokoni awamu ya nne

General / 22nd May, 2023


Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa deni la Taifa kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bwn. Japhet Justine ( katikati ) akigonga kengere kuashiria Uorodheshwaji wa Hati Fungani ( Bond ) ya TMRC sokoni , kwa Awamu ya Nne , Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Dar Es Salaam Stock Exchange ( DSE ) Bi. Mary Mniwasa akiwafuatiwa na Mkurugenzi wa TMRC Bwana Oscar Mgaya.

KAMPUNI ya Utoaji Mikopo kwa Mabenki na Taasisi za fedha kwa ajili ya mikopo wa nyumba Tanzania yaani Tanzania Mortgage Refinance Company ( TMRC ) , Leo Mei 19 , 2023 imefanya Uorodheshaji wa Hati Fungani ( Bond ) yao awamu ya nne , Tukio lililohudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa deni la Taifa kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bwn. Japhet Justine ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi.

Hatifungani hii ya awamu ya 4 imeorodheshwa kwa mafanikio makubwa kwa kuwa ” OVER SUBSCRIBED ” kwa asilimia 12.8 suala ambalo linadhiirisha kwamba wawekezaji wana imani kubwa na TMRC .

Akizungumza baada ya tukio hilo la Uorodheshaji wa Hati Fungani Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa deni la Taifa kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bwn. Japhet Justine ameipongeza sana Taasisi ya TMRC kwa kazi kubwa na nzuri ambayo wanaendelea kuifanya lakini pia kwa kuwa na mwendelezo wa Uorodheshaji wa Hati Fungani zao na kuwaahidi kuwa serikali itakua bega kwa bega nao.

” Niwapongeze sana TMRC kwa mafanikio makubwa maana kutoka Bilioni 10 mpaka zaidi ya bilioni 11.28 ni kiwango kikubwa kwa hiyo niwapongeze sana kwa kazi kubwa mnayoifanya , lakini pia niwapongeze wadau wote walioshiriki hasa wanahisa ambao ni zaidi ya asilimia 69 wakiwa ni wawekezaji mmoja mmoja na makampuni ambayo ni takribani 31 % , niwapongeze sana TMRC kwa kuangalia kwamba Fursa ya kuunga mkono soko letu la nyumba haiishii tu kwa njia ya kutafuta mikopo ya muda mrefu bali mmefikiria kuwatumia Dar Es Salaam Stock Exchange ( DSE ) kama sehemu Muhimu ya kuweza kupata mitaji , niwapongeze sana .

Naye kwa Upande wake Mkurugenzi wa TMRC Bwana Oscar Mgaya amesema kuwa ” Uorodheshaji wa Hati Fungani hii kwa mafanikio haya makubwa ya kupata wawekezaji zaidi ya kiwango kilichotarajiwa inaonyesha kuwa wawekezaji wana Imani na sisi lakini pia inadhiirisha kuwa TMRC inatimiza majukumu yake ya kuweza kupata pesa za kuendeleza soko la nyumba lakini pia katika kuendeleza ukuaji wa soko la hisa na Mitaji , Mpango wetu ni kwamba tutaendelea kuwatumia soko la hisa na mitaji kuweza kupata pesa za kuendeleza soko la nyumba na makazi “

Naye kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Dar Es Salaam Stock Exchange ( DSE ) Bi. Mary Mniwasa  amewapongeza TMRC kwa kupata pesa zaidi kutoka bilioni 10 waliyokuwa wanaitafuta hadi zaidi ya bilioni 11 , ameendelea kuwapongeza zaidi kwa hatua kubwa ya kuorodhesha Hati Fungani 4 katika kipindi cha miezi 12 ambazo zote zikijumuishwa zinakuwa na Thamani ya Tsh. Bilioni 135.5 niwapongeze sana . Alimalizia