Tigo yaboresha mtandao wake kuwasaidia wakulima,wafugaji

Tigo yaboresha mtandao wake kuwasaidia wakulima,wafugaji

General / 6th August, 2024


KAMPUNI ya simu ya mkononi ya Mtandao wa Tigo , imesema imeboresha mtandao huo na kuwa mtandao wenye kasi unaoongoza hapa nchini kwa lengo la kuwasaidia wateja wake kufanya shughuli zao zikiwemo za kilimo,uvuvi na ufugaji.

Aidha imeleta simu janja za bei nafuu ili wakulima,wafugaji na wavuvi hata wenye kipato cha hali ya chini waweze kumiliki simu janja na kufanya shughuli zao kimtandao.

Akizungumza katika maonesho ya wakulima na wafugaji ,Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kati Said Iddy amesema kwa kutumia mtandao wa tigo wakulima na wafugaji wanapata fursa ya kutafuta masoko ya bidhaa zao.

Amesema kupitia mtandao wa tigo ulioboreshwa ,wakulima,wafugaji na wavuvi wanakwenda kuoata taarifa za masoko ya bidhaa zao na bidhaa nyingine wanazohitaji ili kuboresha shughuli zao.

Amewaasa wananchi,wakulima,wafugaji na wavuvi kufika kwenye banda la Tigo ili wakajipatie bidhaa za mtandao huo wenye kasi ikkwemo simu janja aina ya ZTE A34 inayopatikana kwa mkopo wa kianzio cha shilingi 35,000.

David Mazuguni mkazi wa Chahwa wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma ambaye alifika katika banda hilo ameishukuru kampuni hiyo kwa kuwawezesha wananchi wa hali ya chini kumudu kumiliki simu janja.