The Royal Tour Yatizamwa na Watu Bil 1.2
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na
Utalii na Mwenyekiti
wa Kamati ya Rais ya Kuitangaza Tanzania, iliyoratibu maandalizi ya filamu ya
Royal Tour, Dkt. Hassan Abbasi, amesema mwaka mmoja, tangu filamu hiyo izinduliwe hapa nchini,
takribani watu bilioni 1.2 duniani, wameiona au kujihusisha na filamu hiyo
kupitia taarifa za vyombo mbalimbali vya habari.
Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo Aprili 28, 2023
alipokutana na wanahabari jijini Dodoma ikiwa ni mwaka mmoja tangu Rais Samia
Suluhu Hassan alipoizindua filamu hiyo jijini Arusha mwaka jana.
“Mwaka mmoja leo Royal Tour imeleta mafanikio
makubwa sana ikiwemo kuongeza watalii nchini maradufu, mapato ya utalii
kuongezeka maradufu na hata mashirika mbalimbali ya ndege ya kimataifa kuongeza
miruko ya kuja nchini,” alisema Dkt. Hassan Abbasi
Aidha, kumekuwa na
ongezeko la mapato ya utalii maradufu ambapo mapato ya jumla ya sekta
yameongezeka kutoka Dola za Marekani bilioni 1.310.34 sawa na Sh trilioni 3.01
mwaka 2021 hadi Dola za Marekani bilioni 2.527.77 sawa la Sh trilioni 5.82.
Filamu hiyo ni maono ya Rais Samia Suluhu Hassan.
“Mwaka
mmoja uliopita tulizindua Royal Tour na Watanzania waliiona rasmi, wakati
tunatangaza Royal Tour hatukudhani kama tungefikia hapa,” alisema na kuongeza
kuwa taasisi zote kubwa duniani zilizoifanyia ulinganifu na alama Filamu ya
Royal Tour zimeipa alama kubwa pengine kuliko Royal Tour nyingine nane.
Alisema kuwa Mtandao wa TripAdvisor: Mtandao
namba moja duniani katika kutangaza utalii umeipa Royal tour alama 5/5; Mtandao
wa Amazon Video; umetoa alama 4.5/5; na Mtandao wa IMDb; Mtandao namba tatu
duniani baada ya Youtube na Netflix umeipa Royal Tour alama 8.8/10.
Alisema kuwa kwa mujibu wa ripoti ya waandaaji
wa Royal Tour, filamu hiyo si tu imeshaoneshwa katika vituo zaidi ya 300 vya
televisheni vilivyoko kwenye majimbo yote Marekani, lakini tofauti na Royal
Tour nyingine zote, filamu ya Tanzania imetajwa kuwa namba moja kwa kutazamwa
zaidi na vituo vingi vya televisheni kulazimika kuirudia na vinaendelea
kuirudia.
“Kwa mujibu wa ripoti ya Kampuni ya
Peter Greenberg Worldwide (PGW), kawaida kiwango cha kutazamwa filamu za Royal
Tour katika majimbo inakooneshwa hufikia wastani wa asilimia 67, lakini Royal
Tour ya Tanzania imefikisha wastani wa kihistoria wa asilimia 81,” alisema
Alisema kuwa kupitia mafanikio haya Tanzania sasa imepata
morali ya kwenda kimataifa zaidi kuitangaza Tanzania: Royal Tour sio mwisho ni
mwanzo wa kuitangaza nchi kimataifa zaidi hivyo Kamati mwaka mmoja sasa,
imepokea na inaendelea kuchambua “Royal Tours