Tanzania na Urusi kushirikiana kibiashara

Tanzania na Urusi kushirikiana kibiashara

General / 3rd February, 2022

Balozi wa URUSI nchini Tanzania Mhe.Juri Popov (Kushoto) tarehe 2 Februari 2022 ameongoza ujumbe kutoka Urusi uliokutana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi Latifa Mohamed .

 

Lengo ni kujadili mikakati mbalimbali ya ushirikiano wa kukuza biashara baina ya nchi hizo mbili.

 

Mhe.Balozi alieleza kuwa nchi yake imekuwa na ushirikiano wa muda mrefu na hivyo ni muafaka sasa kwa pande zote mbili kuimarisha ushirikiano wa kibiashara.

 

Pamoja na Ushirikiano huo wa kibiashara ,ujumbe huo pia ulieleza nia ya Serikali yake kuwa kati ya Moja ya nchi zinazoshiriki katika mchakato wa kumpata Muandaaji wa Maonesho makubwa ya Dunia maarufu kama Expo ifikapo 2030. Maonesho ya Expo yanayofanyika kila baadaya miaka Mitano na kuleta mataifa yote pamoja kwa lengo kutangaza na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia.

 

Aidha, Bi.Latifa alitumia fursa na kuwafikishia ujumbe wa kutumia Lugha ya *Kiswahili* kama Moja ya Lugha rasmi ya mawasiliano katika Maonesho hayo 2030. wito wangu kwenu, naomba endapo mtapata nafasi hii ya kuwa wenyeji wa Maonesho haya Expo2030 basi Kiswahili iwe Lugha Mojawapo rasmi katika maandalizi yenu alisisitiza Bi.Latifa.

 

Lugha ya Kiswahili ni lugha rasmi kwa nchi za Umoja wa Afrika (AU) na inazungumzwa na nchi nyingi za Afrika. Hivyo ni fursa ya pekee kuitangaza lugha hiyo na utamaduni wake kimataifa.

 

Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi.Latifa Khamis pamoja na wataalam wake amewahakikishia Ushirikiano wa Kibiashara kwa bidhaa za ndani, Sisi tupo tayari kushirikiana na Urusi ili kupanua soko la bidhaa zetu na kutumia fursa zilizopo nchini Urusialiongeza Bi.Latifa.

 

Nchi zingine zinazoomba kuandaa Maonesho ya Expo2030 pamoja na Urusi ni Korea Kusini(Busan), Saudi Arabia(Riyadh), Italia(Rome) pamoja na Ukrain(Odesa)

 

Ujumbe Kutoka Urusi ulioongozwa na Mhe.Balozi Popov ulijumuisha wataalam wengine ambao ni Evgueni Primakov, Alexei Povkovnik,Serguei Klimov , Alexei Bondaruk na Slava Karasev