Tanzania Kitovu cha Biashara Mtandao Afrika Mashariki

Tanzania Kitovu cha Biashara Mtandao Afrika Mashariki

General / 25th November, 2022


Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Posta Tanzania imesaini makubaliano ya kibiashara na Shirika la Posta la Oman katika biashara mtandao kwa lengo la kupanua wigo wa kimataifa wa biashara mtandao huku ikiiwezeshja Tanzania kuwa kitovu cha biashara mtandao katika ukanda wa Afrika Mashariki.

 

Hatua hii inafuatia kusainiwa kwa makubaliano ya awali mwezi mei mwaka huu kati ya Shirika la posta Tanzania na Shirikala Posta la Oman na kutiwa saini na Postamasta Mkuu wa Posta Tanzania Bw. Matrice Mbodo na Postamasta Mkuu wa Posta Oman Bw. Nasser Al Sharji jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye yaliyolenga kukuza biashara za posta kupitia ushirikiano uliopo baina ya mashirika hayo.

 

Hata hivyo hatua hii ya pili imeshuhudiwa na Mhe. Nape jijini Muscat, nchini Oman ambapo yanalenga kukuza biashara mtandao na kuifanya Tanzania kuwa kitovu kwa ukanda wa Afrika Mashariki.