SMZ kuendeleza ushirikiano na NSSF

SMZ kuendeleza ushirikiano na NSSF

General / 23rd September, 2023


Na Iddy Lugendo 


KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ( Zanzibar ) Fatma Hamad Rajab amesema ataendelea kushirikiana bega Kwa bega na Mfuko wa  ili kuhakikisha wanaitangaza NSSF maeneo yote ambayo waliweza kufanya kisiwani Pemba nahatimaye kupata wateja wengi.


Akizungumza wakati akitembelea bana la Mfuko wa hifadhi ya jamii ( NSSF ) kwenye Maonyesho ya sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini Geita Mwaka huu 2023 iliyoambatana nankaulinmbiu isemayo " Matumizi ya Teknolojia sahihi katika kuinua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi Mazingira"


Fatma amesema ataendelea kushirikiana bega kwa bega na  Mfuko NSSF Kwa lengo la kuwapatia wateja weng zaidi na huku akiwaapongeza watumishi wa mfuko wa hifadhi za jamii ( NSSF ) Mkoa wa Geita chini ya Meneja wake Winniel Lusingu kwa uwajibikaji wao katika kuwatumikia wateja wao.


" Nitashirikiana nanyi bega kwa bega ili kuhakikisha NSSF inapata wateja wengi zaidi kama ambavyo waliweza kufanikiwa kisiwani Pemba na tukapata wateja wengi zaidi ambao sasa hivi wanakwenda Dar es salaam au Tanzania kutafuta nyumba na Viwanja, lakini pia nitahakikisha watu wengi wanajiunga na Mfuko wa hifadhi ya jamii ( NSSF ) hadi kieleweke" amesema Fatma.


Aidha aliwapongeza watumishi hao kwa kufanya kazi kwa umoja, mshikamano na upendo, hakika mnapiga kazi nzuri sana, na kinachosababisha ni umoja wao nanhivyo kuwataka kuendelea kuwa wamoja, lakini pia amewataka watumishi hao kuhakikisha wanampa nguvu  Mkurugenzi wao ili aweze kufanya kufanya kazi nzuri zaidi na zaidi ili kuhakikisha NSSF inaendelea kufanya vizuri.


"Lakini pia muwe karibu sana maana mie anasema yeye ni lulu,lakini mie nasema yeye ni dhabhabu, hivyo hiyo Dhahabu muwe nayo karibu sana ili kuhakikisha kazi zote zinakwenda vizuri,lakini mnasaidiana  katika matukio yote ikiwa ya kazi, ikiwa ya kijamii hakikisheni mnashirikiana ili kuhakikisha wote mnafanya kazi kama timu ya pamoja" amesema Katibu Mkuu Fatma.


Aidha Meneja wa Mfuko wa hifadhi ya jamii ( NSSF )  Mkoa wa Geita Winniel Lusingu  amesema Mfuko huo unaangalia Sekta binafsi na Sekta isiyo rasmi, hivyo kuwepo kwenye Maonyesho hayo wako kwa wadau wao muhimu .


" Kuwepo hapa kwenye Maonyesho haya kwakweli ni wadau wetu ambao wanatusaidia kwa kiasi kikubwa sana cha mchango, kwani Ofisi ninkama imehamia hapa , wanacha wakija hapa  wanapata huduma zote  kama wako Ofisini, lakini kwasababu NSSF  tumeenda mbali zaidi  Kiiteknolojia tunahakikisha kwamba wanachama wetu popote wanapo kuwepo  wanaweza kupata huduma  za NSSF kikamilifu nankwanurahisi zaidi" amesema  Winniel Lusingu.