Simba yarejea tena Kileleni, Bocco amlipa Mayele Hat-trik 3

Simba yarejea tena Kileleni, Bocco amlipa Mayele Hat-trik 3

General / 19th November, 2022

Na Rajabu Msangi

Klabu ya Simba SC imerejea tena kileleni kwa alama 27 wakiwa na michezo 12 mara baada ya kufunga mabao 4 -0 dhidi ya Ruvu Shooting FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (NBC) uliochezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo Mchezaji John Raphael Bocco amefunga mabao 3 katika mchezo huo dakika ya 4, 18 na 69 huku bao moja likifungwa na Mlinzi wa timu hiyo, Shomari Kapombe dakika ya 36.

Hii inakuwa ni hat-trick ya kwanza kwenye kikosi cha Simba lakini ikiwa ni ya pili kwenye ligi baada ya Mshambuliaji wa Yanga SC Fiston Mayele kufunga kwenye mchezo wao dhidi ya Singida BS ambapo walipata ushindi wa mabao 4-1

Hata hivyo Simba SC wamerejea tena kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC kwa alama 27 wakiwa na jumla ya michezo 12 na mabao 19 huku Yanga SC wakishika nafasi ya pili kwa jumla ya alama 26 wakiwa na michezo 10 huku Azam akishika nafasi ya tatu kwa alama 26 na michezo 12.