Sakata la Askofu Mwingira Kutaka kuuawa mara tatu, Waziri Simbachawene aagiza Mwingira ahojiwe.

General / 27th December, 2021

Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amemtaka kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam kumtafuta Mtume na Nabii Josephat Mwingira ili kumhoji juu ya tuhuma mbalimbali alizozitoa.

Simbachawene ameyasema hayo leo Jumatatu Desemba 27, 2021 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu masuala mbalimbali.

Hatua hiyo ya Waziri Simbachawene imefuata baada ya kuwepo kwa taarifa mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii zikimnukuu Askofu Mwingira akutoa tuhuma mbalimbali ikiwemo kutishiwa maisha na mali zake kuteketezwa shambani kwake.

Askofu Mwingira amekaririwa akizungumza hayo kanisani kwake wakati wa ibada Jumapili Desemba 26, ambapo alieleza madhila aliyopitia wakati wa utawala wa serikali ya awamu ya tano.