NMB Yatoa msaada wa vifaa tiba Zaidi ya Mil. 26

NMB Yatoa msaada wa vifaa tiba Zaidi ya Mil. 26

General / 23rd January, 2023


Benki ya NMB imetoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya Zaidi ya Shilingi Milioni 26 Wilaya ya Arusha katika kuunga mkono juhudi za Serikali kuboresha huduma za Afya  nchini.


Miongoni mwa msaada huo ni pamoja na vitanda  10 vya kujifungulia kwa kina mama
na  Vitanda 10 vya kulazia wagonjwa wa kawaida.

Kabla ya kukabidhi vifaa hivyo, Afisa Mkuu wa Huduma Shirikishi wa NMB, Nenyuata Mejooli amesema kuwa vifaa hivyo ni moja ya ushiriki wetu katika maendeleo ya jamii na wao kama benki inayoongoza Tanzania, wanao wajibu wa kuhakikisha jamii inayowazunguka inafaidika kutokana na faida wanayoipata.


Aidha aliongezea kuwa Benki ya NMB imekuwa ikipokea maombi mengi sana ya kuchangia katika miradi ya jamii, lakini benki imejikita zaidi katika maeneo ya elimu, afya, na misaada ya hali na mali katika nyakati ngumu kama za majanga na tumekuwa mstari wa mbele kuchangia huduma za kijamii kwa lengo la kurejesha sehemu ya faida yetu kwa jamii.

kwa zaidi ya miaka kumi mfululizo, Benki ya NMB imekuwa ikitenga asilimia 1℅ ya faida yake kama sehemu ya uwajibikaji kwa jamii inayoizunguka.