NMB yatoa Gawio la kihistoria la Shilingi Bilioni 181 Kwa Wanahisa Wake

NMB yatoa Gawio la kihistoria la Shilingi Bilioni 181 Kwa Wanahisa Wake

General / 10th June, 2024

Wanahisa wa Benki ya NMB wameidhinisha gawio la Shilingi Bilioni 181, sawa na shilingi 361 kwa kila hisa moja kwa mwaka unaoishia Disemba 31, 2023.

Azimio hilo limepitishwa leo wakati wa Mkutano Mkuu wa 24 wa Wanahisa wa Benki ya NMB.

Hili ni ongezeko la 26% ukilinganisha na gawio la jumla la Shilingi Bilioni 143.1 tulilolipa mwaka 2022, na kuandika historia mpya ya kuwa gawio kubwa zaidi kuwahi kutolewa na taasisi ya fedha nchini kwa wanahisa wake.

Mafanikio haya ni matokeo ya mazingira mazuri ya kibiashara yaliyowekwa na Serikali yetu, imani ya wanahisa na wateja wetu, juhudi za wafanyakazi wetu na ushirikiano mzuri tulionao na wadau wetu wote.

Tutaendelea kusimamia ahadi yetu ya kudumu katika ukuaji jumuishi na endelevu kwa ustawi wa jamii tunayoihudumia na uchumi wa nchi yetu ya Tanzania kwa ujumla.

Tunawashukuru wadau wetu wote kwa kuwa sehemu ya mafanikio haya.

#NMBAGM2024 #NMBKaribuYako