NMB YAPAMBA MASHINDANO YA SHIMIWI

NMB YAPAMBA MASHINDANO YA SHIMIWI

General / 27th September, 2024

Michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) imefunguliwa rasmi kuzikutanisha timu zinazowajumuisha  watumishi wa serikali kutoka kwenye wizara, taasisi, wakala za serikali, ofisi za wakuu wa mikoa, halmashauri, pamoja na manispaa.


Uzinduzi huu umefanywa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Biteko aliyeambatana na Naibu Waziri Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma pamoja Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Adam Malima.

Uwakilishi wa benki ya NMB ambayo imekabidhi msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. mil.  24.5 umeongozwa na Meneja wetu Mwandamizi wa Mahusiano ya Benki na Serikali, Josephine Kulwa, Meneja Mwandamizi Huduma za Kibenki kwa Serikali, Amanda Feruzi, pamoja na wafanyakazi wengine.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko akisalimiana na Meneja Mahusiano Mwandamizi Kati ya Benki na Serikali, Josephine Kulwa (kulia) pamoja na Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Adam Malima (kushoto) na Meneja Mwandamizi Huduma za Kibenki kwa Serikali Benki ya NMB, Amanda Feruzi wakati wa uzinduzi wa michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) katika uwanja wa jamhuri Morogoro. 
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko akifurahia jambo na naibu waziri wa michezo, utamaduni na sanaa, Hamis Mwinjuma na Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Adam Malima wakati wa uzinduzi wa michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) katika uwanja wa jamhuri Morogoro huku benki ya ikikabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. 24.5milioni.