NMB yaendesha Semina ya Bima kwa Wahariri wa vyombo Habari

NMB yaendesha Semina ya Bima kwa Wahariri wa vyombo Habari

General / 19th July, 2024

Benki ya NMB imesifiwa kwa jitihada zake za kukuza uelewa na elimu ya bima kwa jamii. Pia, vyombo vya habari nchini vimetakiwa kushirikiana na serikali katika kusukuma mbele ajenda hiyo muhimu kwa Watanzania.


Pongezi na wito huo zilitolewa na Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Khadija Said, mnamo Julai 18, wakati akifungua mafunzo ya siku moja kuhusu Huduma za Bima Mtawanyo (BankAssurance) kwa wahariri na waandishi waandamizi wa vyombo vya habari, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.


Bi. Khadija Said alimwakilisha Kamishna wa TIRA kufungua mafunzo hayo, ambayo yalihusisha mada mbalimbali. Mada hizo zilijumuisha "Bima ni Nini," "Benki Wakala wa Bima," "Kazi za NMB Katika Uwakala," na "Huduma za Kibenki na Bima Rafiki kwa Wanahabari." Mafunzo haya yalitolewa na Meneja Mwandamizi wa Bima wa NMB, Martine Massawe.

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Bi. Khadija alisema NMB imechukua hatua kubwa kwa kutenga muda wa kutoa elimu kwa wahariri na wanahabari waandamizi, ambao kwa kutumia vyombo vyao vya habari, wataongeza uelewa na elimu ya bima kwa jamii, ambalo ndio lengo chanya la Serikali.

“Niwapongeze NMB kwa mchango mkubwa katika kukuza uelewa wa elimu ya bima kwa jamii, inachofanya hapa ni kutekeleza Mpango Mkakati wa Serikali na Mpango Mkakati wa TIRA, unaotaka kufikia mwaka 2030, asilimia 80 ya Watanzania wawe na elimu ya bima na asilimia 50 kati ya hao wawe wanatumia Huduma za Bima.

Alibainisha ya kwamba Miongozo ya BenkiBima (BankAsuarance) imetolewa kwa mujibu wa Sheria, Kifungu cha 6(2) na Kifungu cha 11(A na B) ya Sheria ya Bima Sura ya 314, ambacho kinataka Mamlaka kuweka vigezo vya Bima vinavyopaswa kuzingatiwa na Taasisi za Fedha katika utoaji bima.

Khadija alikiri ya kwamba Benki Bima ni sekta inayokua kwa kasi nchini, ikihusisha Sekta ya Fedha na Sekta ya Bima yenyewe, siri ya ustawi na ukuaji huo sio tu suhirikiano baina ya taasisi hizo, bali pia mchango mkubwa wa vyombo vya habari katika kujenga na kuimarisha uelewa kwa jamii