NMB Jiwekee yazinduliwa
Kwa mara ya kwanza nchini, tumezindua rasmi NMB Jiwekee, yenye lengo la kuhifadhi pesa kidijitali kwa ajili ya maisha ya baadae.
Kupitia NMB Jiwekee, mteja ataweza:
➡️ Kuweka kati ya asilimia 1-100 ya kipato kinachoingia kwenye akaunti yake na anaweza kubadilisha muda wowote
➡️ Kuhifadhi hela kwenye NMB Jiwekee kuanzia miaka 5 na kuendelea
➡️ Kuvuna riba shindani na ataipata kila baada ya miezi mitatu
➡️ Kusitisha uchangiaji kwa muda kutokana na mahitaji, bila ya kutoa pesa zake kwenye NMB Jiwekee, na ataweza kuendeleza uchangiaji wakati wowote kupitia NMB Mkononi
➡️ Hakuna kiingilio wala makato
➡️ Kuweka amana katika NMB Jiwekee kupitia mitandao ya simu, benki zingine na mifumo yetu yote.
➡️ Kuangalia salio na taarifa za michango yako kupitia NMB Mkononi.
Uzinduzi huu umeongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu – Mhe. Deo Ndejembi na Afisa wetu Mkuu wetu wa Wateja Binafsi na Biashara- Filbert Mponzi.
Pia, mahojiano yaliongozwa na Millard Ayo huku mada za utunzaji pesa zikitolewa na Lamata Leah pamoja na Masoud Kipanya.