Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita', Zahara Michuzi atoa wito kwa watanzania kutembelea banda la COSTECH

General / 4th July, 2022

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita Zahara Michuzi, ametoa wito kwa watanzania kutembelea banda la tume ya Sayansi na teknolojia nchini Tanzania ( COSTECH) katika maeonesho ya 46 ya Biashara Sabasaba yenye kauli mbiu' TANZANIA MAHALI SAHIHI  PA BIASHARA NA UWEKEZAJI ' Jijini Dar es Salaam kwaajili ya kujifunza vitu mbalimbali vya kibunufu ambavyo vimejikita katika kutatua matatizo ya kijamii.


Michuzi ametoa rai hiyo alipotembelea banda tume hiyo katika maeonesho ya 46 ya Biashara Sabasaba leo Jumatatu Julai 4,2022.


Amesema bunifu hizo zinailetea tija Serikali sambamba na kuiletea fedha za kigeni kwa kuuza bidhaa zilizovumbuliwa na watanzania.


" Wakitembelea banda hili watajifunza bunifu mbalimbali pamoja na kuvumbua vipaji vyao kama wanavyo na kuweza kusaidia na kufika mbali" amesema Zahara .


Ameongeza kuwa yeye kama Mkurugenzi amechagua maeneo muhimu ya kwenda kufanyia kazi kwaajili ya kuongeza tija na kasi ya utendaji kazi katika Halmashauri ya Mji Geita.


Hata hivyo Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa viongozi wengine kutembelea banda hilo kwaajili ya kujifunza teknolojia mbalimbali ambazo zinatumika katika shuguli mbalimbali za kila siku ili kuliletea taifa maendeleo.