Mangungu; Basi la Simba limeuzwa

Mangungu; Basi la Simba limeuzwa

General / 20th January, 2023


Mwenyekiti wa Simba SC Murtaz Mangungu ambaye anamaliza muda wake na anaomba kura za kuendelea kugombea nafasi hiyo kwenye uchaguzi unaotarajia kufanyika Januari 29, Murtaza Mangungu amekiri kuwa basi la timu hiyo limeuzwa na sio bovu kana inavyoelezwa.


Simba ambayo ni muda sasa basi lao limekuwa halionekani huku wakitumia basi dogo 'Coaster' na taarifa ya awali ikithibitisha kuwa basi ni bovu sasa imethibitika kuwa limeuzwa.

"Nashushiwa lawama ambazo sio zangu basi la Simba limeuzwa mimi nikiwa sipo kwenye uongozi sikuwa Mjumbe wa Bodi wala Mwenyekiti wa timu hii kama nilivyo sasa,”

“Lakini baada ya kuingia kwenye uongozi hili suala lilipelekwa kwenye Bodi ya klabu na wajumbe tumelifuatilia na kubaini kuwa limeuzwa kwa kufuata utaratibu," anasema kiongozi huyo ambaye anaiongoza timu hiyo hadi Januari 29 ambayo ni siku ya uchaguzi mkuu.