Katibu Mkuu uwekezaji Dkt. Tausi Mbaga Kida atembelea mradi wa kiwanda cha kuzalisha vifaa vya umeme Elsewedy EA Limited.

Katibu Mkuu uwekezaji Dkt. Tausi Mbaga Kida atembelea mradi wa kiwanda cha kuzalisha vifaa vya umeme Elsewedy EA Limited.

General / 21st March, 2023

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais anaeshughulikia Uwekezaji Dkt. Tausi Mbaga Kida ametembelea mradi wa Kiwanda cha kuzalisha vifaa vya umeme Elsewedy EA Limited kilichopo wilaya ya  Kigamboni, jijini Dar es Salaam leo 21 Machi, 2023.

Katika ziara hiyo Dkt. Kida aliambatana na  wafanyakazi wa TIC wakiongozwa na  Bw. Revocatus Rasheli Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji kwa Wawekezaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Akieleza malengo ya ziara hiyo Dkt. Kida amesema Mradi huo ni moia ya matunda ya miaka miwili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani alipoingia tu madarakani alitembelea nchini Misri na kualika wawekezaji kuja kuwekeza hapa nchini. Aidha wawekezaji hao walianza utekelezaji wa mradi huo Desemba 2021 na mpaka sasa wamewekeza zaidi ya dola milioni 40 za kimarekani.

Hata hivyo Dkt. Kida amesema kuwa Kiwanda hicho kinasafirisha bidhaa zake nchi mbalimbali zikiwa na nembo ya Tanzania, baadhi ya nchi hizo ni Africa ya Kusini, Kenya, Sudan ya Kusini, Rwanda na zinginezo , hivyo kutuongezea fedha za kigeni na kupunguza matumizi ya fedha za kigeni kununua bidhaa hiyo nje ya Tanzania.

Kwa upande wake Mkurugenzi  Mkuu wa Elsewedy Bw. Ibrahim Qamar amesema Kampuni yao imeamua kufanya Tanzania kuwa makao makuu ya uwekezaji Africa. “Uwekezaji huu umetoa ajira za moja kwa moja 400, wafanyakazi wa siku ni zaidi ya 50 na mkataba 600.” amefafanua  Bw. Qamar

Kiwanda hicho kwa sasa  kinatengeneza Cable na Transfoma na kinazalisha pia bidhaa za vifaa vingine vya umeme kama vile cable za paneli za Nishati ya jua kwa mahitaji maalum.