Kampuni ya TTCL yasaidia wagonjwa wa saratani Ocean Road

Kampuni ya TTCL yasaidia wagonjwa wa saratani Ocean Road

General / 20th March, 2023

Afisa Uhusiano wa TTCL, Bi. Adeline Berchimance (wa tatu kushoto) kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Shirika hilo, Mhandisi Peter Ulanga akikabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya wagonjwa wanaopata matibabu katika Taasisi ya Saratani Ocean Road ya jijini Dar es Salaam. Anayepokea kulia ni Muuguzi Msimamizi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road ya jijini Dar es Salaam, Bw. Mwanga Muhoka.

 

Baadhi ya Wafanyakazi Wanawake wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wakikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya wagonjwa wanaopata matibabu katika Taasisi ya Saratani Ocean Road ya jijini Dar es Salaam.

Afisa Uhusiano wa TTCL, Bi. Adeline Berchimance akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Shirika hilo, Mhandisi Peter Ulanga mara baada ya kukabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya wagonjwa wanaopata matibabu katika Taasisi ya Saratani Ocean Road ya jijini Dar es Salaam. 


Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road ya jijini Dar es Salaam, Bw. Justine Chambo akizungumza kuishukuru TTCL mara baada ya kupokea msaada huo.


Muuguzi Msimamizi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road ya jijini Dar es Salaam, Bw. Mwanga Muhoka akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo.

WAFANYAKAZI Wanawake wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya wagonjwa wanaopata matibabu katika Taasisi ya Saratani Ocean Road ya jijini Dar es Salaam. Wafanyakazi hao wametoa msaada huo ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani, ambapo pamoja na mambo mengine huyatumia maadhi kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo  kuwaona wagonjwa na kuwafariji. 


Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo, Afisa Uhusiano wa TTCL, Bi. Adeline Berchimance kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Shirika hilo, Mhandisi Peter Ulanga, alisema wanatambua kazi kubwa inayofanywa na Taasisi ya Saratani Ocean Road hivyo wameguswa kujitoa kwa kufariji wagonjwa.


"...Tunaushukuru uongozi wa Taasisi hii kwa juhudi mbalimbali mnazoziweka katika kuhakikisha wagonjwa wanaofikishwa hapa wanapatiwa huduma stahiki huku mkitanguliza upendo na moyo wa majitoleo ili kuwarejeshea tabasam tena, tunatumia fursa hii pia kuwapongeza wanawake wote katika Taasisi hii kwakutumia umama wao kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kama akina mama ndani ya taasisi na kama watumishi kitaaluma kutoa huduma kwa wahitaji hawa," alisema Bi. Berchimance.


TTCL imetoa wito kwa wadau, mwananchi mmoja mmoja, Taasisi na Kampuni mbalimbali kuendelea kujitoa kwa misaada ya hali na mali kwa Taasisi ya Ocean Road ili kuiunga mkono kwani inafanya kazi kubwa ya kuhudumia wagonjwa hao nchini huku ikiwa na mahitaji mengi yanaoitaji ushirikiano wa kila mwenye kuguswa.

Miongoni mwa vitu vilivyo kabidhiwa ni pamoja na Tumekuja Pampasi Katoni 30, Sabuni ya unga viroba 7, mafuata ya kupaka katoni 4, Sabuni ya mche katoni 7 na Dawa ya meno katoni 10 , vyote vikiwa na thamani ya zaid ya milioni nne.


Afisa Uhusiano wa TTCL, Bi. Adeline Berchimance (wa tatu kushoto) kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Shirika hilo, Mhandisi Peter Ulanga akikabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya wagonjwa wanaopata matibabu katika Taasisi ya Saratani Ocean Road ya jijini Dar es Salaam. Anayepokea kulia ni Muuguzi Msimamizi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road ya jijini Dar es Salaam, Bw. Mwanga Muhoka.


Afisa Uhusiano wa TTCL, Bi. Adeline Berchimance (kushoto) akisalimiana na Muuguzi Msimamizi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road ya jijini Dar es Salaam, Bw. Mwanga Muhoka kabla ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya wagonjwa wanaopata matibabu katika Taasisi ya Saratani Ocean Road ya jijini Dar es Salaam.