Fursa za ufadhili wa Masomo

Fursa za ufadhili wa Masomo

General / 25th February, 2022

Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki imepokea fursa za ufadhili wa masomo (scholarship) ya muda mrefu katika kada mbalimbali kutoka Serikali ya Thailand kwa mwaka wa masomo wa 2022-2023

 

Fursa za masomo zilizotolewa zinahusisha mafunzo ya Shahada ya Kwanza, Mafunzo Shahada ya Uzamili (Master's Program) na Shahada ya Uzamivu (PhD).

 

Taarifa zaidi kuhusu fursa mbalimbali a mafunzo haya zinapatikana kupitia kiunga cha mtandao https:/bit.ly/3J6UYg3 na tovuti www.admissions.au.edu

 

Wizara inawahimiza Watanzania wenye sifa kuchangamkia fursa hizi za masomo zilizotolewa.